Uongozi Wa Mwl. Nyerere

Uongozi Wa Mwl. Nyerere

by Pius Msekwa

PDFFree
Literature
Form VI
160 pages
Pius Msekwa

Yaliyomo katika kitabu hiki ni kumbukumbu ya maisha yangu ya kazi katika utumishi wangu wa umma katika kipindi ambacho Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alikuwa Kiongozi Mkuu wa Taifa la Tanzania. Azma yangu ya awali ilikuwa ni kuandika kumbukumbu ya miaka yote hamsini mfululizo ya uongozi na utumishi wangu kwa umma. Hata hivyo, nilibaini kwamba, kazi hiyo ingekuwa ni kubwa mno na ingechukua muda mrefu zaidi kuikamilisha. Baada ya kubaini hilo na kushauriwa na baadhi ya wenzangu, hatimaye, nikaamua kwamba, kwa kuwa, zaidi ya nusu ya kipindi hicho nilifanya kazi kwa karibu sana na Baba wa Taifa, ingefaa zaidi niandike kumbukumbu zinazohusu kipindi cha uongozi na utawala wa Mwalimu Julius K. Nyerere na kipindi cha utumishi wangu chini ya utawala huo. Kwa hiyo, kitabu hiki kinaishia katika kuweka kumbukumbu ya utumishi wangu katika kipindi kile tu nilichofanya kazi chini ya uongozi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Rate this ebook